Jamii ya kiislamu inaomboleza kifo cha sheikh Amir Hassan Zani aliyefariki asubui ya leo nyumabni kwake eneo la Likoni.

Sheikh Zani alikuwa pia mwanaharakati wa kidini na pia Mkurugenzi wa Walimu wa Madrasa.

Sheikh Zani amezikwa leo huko Kikoneni, Kaunti ya Kwale.

Mwenyekiti wa KEMNAC sheikh Juma Ngao anatoa kauli yake kuhusiana na kifo cha sheikh Zani.


Ngao amemtaja marehemu kuwa alikuwa kiongozi shupavu wa dini.