Usalama wa wanafunzi katika shule ya upili ya wasichana ya Mwanambeyu iliyoko kaunti ya Kwale upo hatarini endapo ujenzi wa ua utakosa kukamilika.

Hii ni kulingana na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Joyce Mbulo anahofia usalama wa wanafunzi kutokana na visa vya uhalifu vinavyotekelezwa kufuatia ukosefu wa ua katika shule hiyo.

Mbulo sasa anaomba msaada kutoka kwa serikali kuu, Ile ya kaunti na wahisani mbalimbali wa kujengewa ua ili kuimarisha hali ya usalama katika shule hiyo.

Mbulo ameweka wazi kuwa usimamizi wa shule hiyo umeshindwa kukamilisha ujenzi wa ua hilo kufuatia ukosefu wa fedha.