Serikali ya kaunti ya Mombasa inalenga kubadili vitengo 16 vya usimamizi wa fuo za bahari yaani BMU hapa Mombasa kuwa vyama vya ushirika.

Kulingana na gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ni kwamba tayari BMU 6 kati ya 16 zimebadilishwa kuwa vyama vya ushirika huku akifanya mchakato wa kubadili BMU 10 zilizosalia.

Akizungumza hapa Mombasa gavana Nassir amesema serikali ya kaunti imetenga takribani shilingi milioni 100 kusaidia vyama hivyo.