Wazee wa mitaa na wakaazi eneo la Likoni wanaishi kwa hofu kufuatia vitisho kutoka kwa vijana wanaoendelea uhalifu eneo hilo.

Wakizungumza na Angazo la Rahma, baadhi ya wakaazi na wazee wa mitaa kutoka Likoni ambao hawakutaka majina yao yatajwe wamelalama kukosekana kwa ushirikiano miongoni mwao na wakuu wa usalama.

Sasa wakaazi wa eneo hilo wameilaumu idara ya usalama kushirikiana na wanachama wa vikundi hivyo, hali ambayo inapelekea vijana wahalifu kuachilia pindi tu wanapokamatawa na kupelekwa katika vituo mbali mbali vya usalama katika eneo hilo.

Wamedai kwamba wengi wa washukiwa huachiliwa bila kufikishwa mahakamani baada ya kutoa hongo kwa wakuu wa vituo vya polisi na hivyo kupelekea kuachiliwa huru magenge ya vijana hao kurudi kuangaisha wakaazi na hata kulipiza kisasi kwa waliowashtaki.