Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amewataka baadhi ya viongozi nchini kuacha kumuekea lawama kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kwa masuala ya serikali.

Akizungumza hapa Mombasa Nassir amesema haileti natija nzuri kwa viongozi kumtwika mzigo kinara huyo wa ODM ikizingatiwa kuwa hayuko katika serikali.

Kulingana naye Raila ni kiongozi mwenye busara na baba wa ugatuzi,akisema amejitolea kupigana ili kuona kuwa taifa la kenya ni la demokrasia.

Aidha amesema Raila amekuwa kielelezo chema kwa viongozi kwa kuwahimiza wajumbe kupigana na suala dhidi ya kupanda kwa ushuru wa bidhaa ya mafuta na sheria kuhusiana na usalama.

Hata hivyo amempigia debe kinara hoyu akisema ni mkombozi wa dhulma zinazofanyiwa wananchi na anafaa kuwa rais wa jamhuri ya taifa la kenya.