Hali yamasomo inaendelea kutatizika katika eneo la Ganze kaunti ya Kilifi kutokana na makali ya njaa ambayo inaendelea kuwakumba wakazi wa eneo hilo.

Radio Rahma ambayo imezuru maeneo mengi ya Ganze imeweza kubaini kuwa baadhi ya wanafunzi wamekosa masomo yao kutokana na ukosefu wa chakula.

Mwalim Mkuu wa shule ya msingi ya Mlungu wa Mawe Simon Mwachoo amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakiishi kwa mlo mmoja kwa siku jambo ambalo amebaini kuwa linarudisha nyuma hali ya masomo.

Kulingana na Mwachoo serikali na wahisani wanapaswa kuingilia kati ili waweze kupeleka chakula cha msaada kwa wakazi hao.

Naye mbunge wa eneo hilo Teddy Mwambire amemtaka waziri wa wizara ya ugatuzi nchini kutembelea eneo la Ganze na kuwapa msaada wa chakula wananchi hao ili wasije wakaaangamia.