Chama cha Wamiliki wa matatu nchini Matatu Owners Association sasa kinawalaumu waajiri kwa kutowapatia muda wa kutosha madereva wao ili wapumzike.

Mshirikishi wa Chama hicho Kanda ya Pwani Salim Mbarack Salim amesema wamiliki hao wa matatu wamechangia pakubwa katika ajali za barabarani kutokana na madai kuwa huwalazimisha madereva wao kuendesha magari kwa muda mrefu bila kupumzika.

Mbarack amesema ni sharti kwa waajiri katika sekta ya uchukuzi kuzingatia masharti ya trafiki sawa na sheria za leba ili kuhakikisha usalama barabarani.

Wakati uo huo, Mbarack vile vile amewahimiza madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani kila mara na hasa msimu huu wa sherehe ili kuhakikisha abiria wao wanafika salama katika safari zao mbalimbali.