Licha ya kinara wa ODM Raila Odinga kushindwa kuweka wazi wa kumuidhinisha atakaye wania kiti cha ugavana kaunti Mombasa kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2022, Odinga amemtaja Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ambaye anawania kiti hicho na yule wa Likoni Mishi Mboko kama miongoni mwa wajumbe wa ODM walio na bidii ya kazi katika bunge la kitaifa.

Kulinga naye viongozi hao wawili wamekuwa mstari wa mbele kukiimarisha chama cha ODM kwa kutoa hamasa kwa jamii mashinani kuhusu umuhimu wa chama hicho na hata kupeleka miswada bungeni pindi wanapoagizwa na chama.

Aidha kwenye ziara yake hapa Mombasa Odinga alitumia nafasi hio kujipigia debe kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Hata hivyo amewataka wananchi kujitahadhari na viongozi wenye tamaa za fisi na kuepuka kubadili vyama.