Wakaazi wa eneo bunge la kinango huko kaunti ya Kwale wamehimizwa kujitokeza na kujisajili kama wapiga kura ifikapo Januari mwaka ujao wakati wa zoezi hilo litakaporegelewa tena.

Mwanaharakti wa maswala ya kijamii na ambaye pia anawania kiti cha uwakilishi wadi ya Macknon Road Hussein Mugandi Kaingu amewahimiza wakaazi hao kujitokeza na kujiandikisha wakati wa zoezi hilo linapotarajiwa kuregelewa.

Akizungumza katika kaunti ya Mombasa Mgandi amedokeza kuwa eneo hilo lilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyosajili idadi ndogo ya wapiga kura kwenye zoezi lililopita.

Aidha Mgombea huyo anasema kuwa idadi ya ndogo ya wapiga kura katika eneo hilo ilichangiwa pakubwa na vifaa vya tume ya IEBC ambapo anasema kuwa katika vituo vingi vilikuwa vikileta hitilafu kila mara na kuitaka tume hiyo kuwa na vifaa ambavyo havitakuwa na hitilafu hali anayoitaja kuwa watu watakuwa wakihudumiwa kwa muda mfupi.

Wakati uo huo amewaomba wakaazi wa eneo hilo kuwa macho na kuchagua viongozi wenye sera ambao watashuhulikia maslahi yao.