Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameweka wazi kuwa atafanya kazi pamoja na maafisa tawala katika wadi mbali mbali kaunti ya Mombasa.

Akizungumza kwenye kikao na baadhi ya maafisa hao katika ukumbi wa Al-Ihshaani wadi ya Tudor hapa Mombasa Nassir ameeleza haja ya kufanya kazi pamoja na maafisa tawala bila ya uwepo wa ubaguzi wa rangi kabila au dini ili kuendeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika jimbo la Mombasa.

Nassir ambaye yuko kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha ugavana kaunti ya Mombas amewataka maafisa hao kusambaza Amani kwa jamii zilizoko mashinani msimu huu ambapo kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 zimeanza kushamiri.

Wakati huo huo Nassir amewaomba maafisa hao kumuunga mkono katika kinyang’anyiro cha kutafuta nyadfa ya ugavana kaunti ya Mombasa.