Baraza kuu la ushauri kwa waislamu nchini KEMNAC limeitaka tume ya uwiyano na utangamano wa kitaifa NCIC kupigania usawa hasa katika maswala ya ugavi wa nafasi za ajira nchini.

Mwenyekiti wa kitaifa wa baraza hilo Sheikh Juma Ngao amesema tume hiyo imefeli katika kupigania usawa kwa Wakenya wote katika ugavi wa nafasi za ajira.

Akizungumza na wanahabari, Sheikh Ngao amesema kwamba ni kutokana na ubaguzi huo wa nafasi za kazi na wakaazi wa Pwani hasa vijana huhisi kutengwa na Serikali ya kitaifa.

Ameongeza kuwa kwa sababu hiyo ndipo kumekuwepo na mchipuko wa makundi mbalimbali kwa lengo la kupigania haki zao msingi.

Kiongozi huyo wa kidini amesisitiza kwamba ni sharti kuwe na suluhu ya kudumu kuhusu suala la ajira ili kuondoa utata wa ubaguzi wa kijamii na kikabila humu nchini.