Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ametoa wito kwa jamii nchini kuwa macho na kutoa ripoti pindi tu wanaposhuhudia matukio ya utekaji nyara.

Akitoa wito huo kwa wakaazi hapa Mombasa Nassir amewataka wakaazi kuacha kulinyamazia suala hilo na kulichukulia kama suala la kawaida na kuwaachia jukumu hilo kwa viongozi badala yake washirikiane pamoja ili kuona kuwa visa vya aina hiyo vinakomeshwa.

Nassir ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wakaazi wa Pwani ameeleza haja ya kuongezwa kwa kamera za CCTV katika maeneo mbali mbali hapa Mombasa ili kusaidia kumilika matukio mbali mbali ya uhalifu.