Wanasaikolojia katika kuanti ya Kilifi wamesema kuna haja ya watu waliopatikana na hatia za dhulma za kijinsia na kingono kupewa ushauri nasaha sawa na wale waliodhulumiwa.

Mwanasaikolojia Anisa Menza amesema kuwa jamii hukosa kuwakubali pindi wanapomaliza adhabu zao za vifungo gerezani na hili huchangia pakubwa kwa watu hao kurudia makosa hayo tena.

Anisa amesisitiza kuwa mwathiriwa anafaa kupewa ushauri hata baada ya haki kupatikana sawia na mhalifu.

Mwanasaikolojia huyo ameitaka jamii kujua chanzo cha mhalifu kufanya uhalifu kwani huenda ikawa analipiza kisasi.