Baadhi ya wakaazi wa nyumba za kupanga mtaa wa mabanda eneo la Tudor wamenusurika baada ya nyumba walimuokuwa wakiishi kuangukiwa na Mti mkubwa aina ya Mwarubaini.

Kulingana na msimamizi wa nyumba hizo Faith Peter ni kwamba mti huo ulianguka mwendo wa saa sita mchana wakati baadhi ya wapangaji walikuwa nje kutafuta riziki.

Aidha Faith amesema kuwa baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya vyumba hivyo viliharibika.

Kadhalka Faith amesema hakuna mwenye aliyejeruhiwa kwenye mkasa huku takribani vyumba 12 ikiwemo choo vikiharibiwa.

Hata hivyo wametoa shukran kwa Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kwa kufika mapema na kuwapa pole.