Kamishna wa kaunti ya Mombasa Lukas Katee Mwanza amewataka wanasiasa kufanya kampeni zao kwa amani bila kuchochea vurugu.

Vilevile amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa hasa vijana kuepuka wanasiasa ambao wana malengo ya kuwatumia ili kuzua vurugu kwenye mikutano ya wapinzani wao.

Akizungumza kenye mkutano wa amani katika eneo bunge la Kisauni, Mwanza amesema kuwa tayari mikakati mwafaka imewekwa ili kuona kuwa amani imedumishwa wakati huu kabla na hata baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka huu.

Amesema kuwa kuwepo kwa amani kutasaidia zaidi katika kuimarisha uchumi wa Mombasa ambao kwa kwa sasa umeanza kuimarika tangu kuzuka kwa janga la Covi-19.

 Mwandishi:Ibrahim Mudibo