Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewataka wakaazi kushirikiana na machifu na kutoa ripoti za wageni wasiowatambua vijijini mwao msimu huu ambapo kampeni zinaonekana kushika kasi humu nchini kwa usalama wao.

Kulingana na msaidizi wa kamishna wa Kwale eneo la Kinango Charles Wesamba baadhi ya wageni sio wakuhubiri amani ila ni wa kuhujumu amani na kuwatishia wenyeji kujitokeza kutimiza haki yao ya kupiga kura.

Amesisitiza kuwa ni sharti wageni wafike kwa afisi za machifu kwa utambulishi ili kuhakikisha usalama na amani vijijini.