Serikali ya kaunti ya Kwale kwa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu imezindua mradi wa kuzisaidia familia zilizoathirika na makali ya ukame katika kaunti hiyo.

Naibu gavana wa Kwale Fatuma Achani ameeleza mradi huo unalenga kutoa pesa kwa wananchi ambapo takriban familia 1500 zinatarajiwa kupokea shilingi 5467.

Vilevile kununua mifugo kutoka kwa wafugaji, kuchinjwa na kupewa wananchi kama chakula badala ya mifugo kuathirika zaidi au kufariki

Hata hivyo amesema kuwa wanaendeleza miradi ya ujenzi wa mabwawa kama suluhisho endelevu kwa ajili ya kupambana kiangazi.

Kwa upande wake Dkt Asha Mohammed katibu mkuu msalaba mwekundu ameafiki kukosekana kwa mvua takriban misimu 3.

Ameongeza kuwa ifikapo mwezi machi watu Milioni 2.8 nchini watakua wameathirika zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Wakati huohuo amewahimiza wakaazi wanaopokea msaada huo kutumika ipasavyo.

Mbogo mwakudza na Rehema Kea wakaazi wa kijiji cha mbuguni mbuguni ni baadhi ya waliopokea msaada huo.