Ubabe wa kisiasa huenda ukashuhudiwa hapo kesho kwenye ziara ya kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Hii ni baada ya mgogoro kuibuka baina ya wafuasi wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi na wale wa chama cha PAA kinachoongozwa na gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi.

Naibu mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi Joseph Chilumo amewambia wanahabari kuwa ziara ya Raila ni ya chama cha ODM pekee wala sio azimio.

Naye kiongozi wa chama cha Pamoja African Alliance Amason Kingi amesema kuwa ziara ya Raila Odinga katika kaunti ya kilifi ni ya azimio wala sio ya chama cha ODM.

Kulingana na Kingi chama cha PAA kitajumuishwa kikamilifu kwenye ziara hiyo baada ya kuhakikishiwa na kinara wa chama cha ODM kuwa ziara yake ni ya azimio.

Kinara huyo wa odm anatarajiwa kuzuru eneo la Bamba,Mariakani,Kaloleni na Mazeras hapo kesho.