Wavuvi kutoka eneo la Shimoni wangali wanapinga vikali mradi wa ujenzi wa bandari ya Shimoni kwa madai ya kuathirika katika shughuli zao.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Rishad Ikki, wavuvi hao wameitaka serikali ya kitaifa kuzingatia athari ya utekelezaji wa mradi huo katika eneo hilo.

Kufuatia hayo Kamishena wa Kwale Gideon Oyagi amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuunga mkono mradi wa ujenzi wa bandari ya Shimoni katika eneo bunge la Lungalunga.

Akizungumza huko mjini Kwale, Oyagi amewataka wakaazi eneo hilo kushirikiana na serikali ya kitaifa ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.

Oyagi amesema kwamba mradi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni utawanufaisha wakaazi katika maswala ya ajira na uchumi.