Kinara wa Odm Raila Odinga ameahidi uteuzi wa haki na usawa katika kura za mchujo baina ya wagombea wa kiti cha ugavana wa Mombasa kati ya Abdulswamad Shariff Nassir na mfanyibiashara Suleiman Shahabali.

Amewataka wawili hao kukubali matokeo yatakavyokuwa na kushirikiana kuendeleza gurudumu la chama cha ODM.

Ameyasema haya baada ya wapinzani wa mfanyibiashara Suleiman Shahbal ambaye anagombea kiti cha ugavana akishindana na mbunge wa mvita Abulswamad Shariff Nassir kaunti ya Mombasa kujaribu kuzua vurugu kwenye mkutano wa Azimio La Umoja.

Hii ni baada ya wakaazi wa Mombasa kuonyesha mapenzi kwa Nassir hali ambayo mpinzani wake Shahbal alionekana kutofurahishwa na kutaka kuonyesha ubabe wake.

Ni hatua ambayo ilimlazimu kinara wa ODM Raila Odinga kuingila kati na kusuluhisha tatizo hilo huku akiahidi uteuzi sawa wa chama kwa wawili hao.

Hata hivyo amewataka mwenye atashindwa kati yao akubali na aunge mkono mwenzake ifikapo uchaguzi mkuu.