Mpango kabambe umeanzishwa na serikali ya kaunti ya Kilifi kwa ushirkiano na shirika la Start up Africa ili kuhakikisha kuwa vijana katika vyuo vya kiufundi katika kaunti hiyo wanapata mafunzo thabiti.

Kwenye kongamano la maonyesho ambalo limefanyika katika chuo kikuu cha pwani,waziri wa elimu katika kaunti hiyo Rechael Musyoki amesema kuwa vyuo vya kiufundi vinaendelea kuwapa mafunzo vijana ili wawe na ujuzi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Nyanja ya kiufundi.

Kulingana na Rechael,vyuo hivyo viko na takriban wanafunzi elfu tano mia nne ambao wanaendelea kupata mafunzo.

Naye mkurugenzi wa shirila la Start up Africa Erustus Mungare amesema kuwa shirika hilo limeshirikiana na serikali ya kaunti hiyo ili kuwapa mafunzo zaidi wanafunzi kwenye vyuo hivyo.

Kulingana na Erustus hatua hiyo itawezesha vijana kupata mapato kupitia ujuzi wao na kujiepusha na maswala ya kiuhalifu.