Usafiri katika bara bara ya Miritini changamwe umesitishwa kwa muda baada ya wahudumu wa boda boda kufunga bara bara hiyo kutokana na vumbi katika eneo la kona ya reli.

Akiongea wakati wa mandamano ya Amani katika eneo hilo msemaji wa boda boda katika eneo la Jomvu Peter Karioki amesema kuwa mwanakandarasi wa bara bara hiyo alisimamishwa na haijulikani itaisha lini.

Hata hivyo baadhi ya wahudumu na wafanya biashara katika eneo hilo la kona ya reli wamesema kuwa vumbi hilo limewaathiri pakubwa kibiashara.

Kwa upande wake mbunge wa Jomvu Badi Twalib amekemea vikali hatua ya wanakandarasi na Kenha kuona kwamba wanazingatia sharia za ujenzi.