Baraza la kusimamia maslahi ya watu wenye walemavu nchini likishirikiana na tume huru ya uchaguzi nchini IEBC limeandaa mikakakati ambayo itawezesha jamii hiyo kupiga kura kwa njia ya usalama.

Akiongea na mwanahabari wetu, mratibu wa mipango wa baraza hilo kaunti ya Mombasa Juliet Ruwa amesema kuwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura ni haki ya kila mkenya aliye na kadi ya kura licha changamoto mbalimbali ikiwemo ya kimaumbile.

Amesema kuwa tayari baraza hilo limeweka mikakakti ya kutosha ikiwemo vifaa vinavyotumika na jamii hiyo ili kuhakikisha kuwa watu wenye wenye ulemavu vilevile wanashiriki katika zoezi la kupiga mwezi Agosti mwaka huu bila ya kupata matatizo yoyote.

Wakati uo huo amewahimiza watu wa jamii hiyo wenye ari ya kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi kujitokeza na kushindania nyadhifa hizo.

Vilevile amewataka wale ambao bado hawajajisajili kama wapiga kura kufika katika afisi za tume ya IEBC na kujisajiliwa ili waweze kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Mwandishi:Ibrahim Mudibo