Madereva wa malori ya masafa marefu hapa nchini, wameshauriwa kujiunga na vyama vya ushirika ili wakabiliane na changamoto zinazowakumba wanapokuwa kazini.

Akiongea na mwanahabari wetu Mwenyekiti wa madereva hao ukanda wa Pwani Roman Waema, amesema kwamba madereva hao wanapitia changamoto nyingi ikiwemo, mishahara duni, ukosefu wa usalama miongoni mwa changamoto nyinginezo.

Amedokeza kuwa licha ya wengi wao kupitia masaibu kazini, hukosa kushughulikiwa kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Waema aidha amesistiza ushirikiano baina ya wadau husika katika sekta hiyo ili kuhakikisha wanapata wanachama wengi zaidi na kutetea maslahi yao.

Mwandishi:Ibrahim Mudibo