Seneta wa Bungoma, Moses Wetangula, amepuuza ripoti kwamba alikuwa kwenye mkutano na aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga.

Katika taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter, kiongozi huyo wa chama cha Ford Kenya amekanusha madai kwamba alikuwa akikutana na mwenzake wa chama cha ODM ili kuafikia makubaliano ambayo yangemfanya aondoke kwenye vuguvugu la Kenya Kwanza  na kujiunga na Azimio La Umoja.

Mshirika huyo wa zamani wa Raila ametaja  kuwa bado yuko Kenya Kwanza na alikuwa akifanya mazungumzo na baadhi ya wanachama wa chama chake katika makao makuu.

Ripoti za kukutana na Wetangula na Raila ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii asubuhi ya Ijumaa, Machi 25, huku wengi wakihoji ukimya wake.