Chama cha ODM kinafanya mchujo wa wagombea wa chama hicho hii leo kaunti ya Kwale.

Katika kura hizo za mchujo ni ikiwemo za wawakilishi wadi pamoja na mbunge wa msambweni.

Kinyang’anyiro kikali kinatarajiwa katika mchujo wa kiti cha ubunge wa msambweni ambapo kuna wagombea watano waliojitokeza.

Wagombea hao ni Sharlet Mariam,Ali Mwakulonda,Charles Bilali,Mahmood Shee na Bashir Kilalo.

Maeneo yaliyo na kura za mchujo wa wawakilishi wadi ni ikiwemo wadi ya Tiwi iliyo eneo bunge la Matuga, wadi za Gombato Bongwe, Ukunda na Kinondo zilizo eneo bunge Msambweni.

Kati ya waliopata tiketi ya mojamoja ni ikiwemo Hamadi Boga katika kiti cha ugavana, Zuleikha Hassan ubunge wa Kinango, Hassan Mwanyoha wa Matuga na Issa Boy katika kiti cha useneta na Fatuma Masito katika kiti cha mwakilishi wa kike.