Mshirikishi wa chama cha Odm kaunti ya Kwale James Nyakiti amesema kwamba wamerekebisha matatizo yaliyosababisha zoezi la mchujo kuanza kuchelewa.

Akizungumza na wanahabari katika eneo la Mwakigwena Nyakiti amewataka wagombea kuondoa wasi wasi kuwa kuna njama ya wizi wa kura.

Aidha amesema kwamba wanafanya zoezi hilo kwa haki na usawa.

Kwa upande wao waliojitokeza kupiga kura miongoni mwao akiwa mwalimu Ali amesema kwamba ameridhishwa na zoezi hilo jinsi linavyoendelezwa licha kuanza kuchelewa.