Ukosefu wa fedha za kutosha kuendeleza shughuli za kisiasa pamoja na vitisho kutoka kwa wanasiasa wakongwe ndio chanzo kikuu cha vijana wengi kususia kuwania viti vya kisiasa hasa katika ukanda wa Pwani.

Kauli hii imetolewa na mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wadi ya Chaani katika eneo bunge la Changamwe hapa kaunti ya Mopmbasa David Musyoki.

Amesema kufuatia ubabe huo wa kisiasa ndio imekuwa sababu kuu ya maendeleo duni katika baadhi ya maeneo hapa Pwani huku akitaja kuwa eneo la Chaani ni mojawapo ya eneo ambalo limekosa miundomsingi bora ya kuboresha maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Huku zoezi la mchujo wa vyama unapokaribia, Musyoki amekitaka chama cha ODM kuandaa zoezi huru na kwamba endapo halitakuw huru huenda likapelekea chama hicho kupoteza wafuasi.Aidha amesisitiza haja ya vijana kupewa nafasi za uongozi ili kujiwakilisha wenyewe.

Mwandishi:Ibrahim Juma Mudibo