Bodi ya kitaifa ya Chama cha ODM ina andaa zoezi la mchujo wa wawaniaji wa wadhfa wa wakilishi wadi hii leo hapa Mombasa.

Akizungumza na wanahabari baada ya kukutana na wawaniaji hao kamishna wa bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya chama cha ODM Richard Tairo amesema kwamba mikakati na mipangilio ya zoezi hilo imekamilika.

Tairo amesema kwamba katika zoezi hilo kuna zaidi ya wawaniaji 160 wa wadhfa wa uwakilishi wadi watakaoshiriki mchujo katika vituo 90 ambavyo vitatumika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa ODM kaunti ya Mombasa Mohammed Hamid Khamis, amewataka wagombea hao kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na bodi ya uchaguzi ya chama hicho ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa usawa.

Hamid aidha amewaonya wawaniaji hao dhidi ya kuchochea vurugu na ghasia wakati wa zoezi hilo na kwamba chama hicho kitamchukulia hatua za kinidhamu yoyote atakaenda kinyume na sheria na kanuni za chama kwa kuzuwa vurugu wakati wa zoezi hilo.

Mwandishi:Ibrahim Juma Mudibo