Serikali ya kitaifa na kaunti zatakiwa kushirikiana kuwawezesha wavuvi kwa vifaa vya kisasa

Ipo haja ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushirikiana kuhakikisha inawekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kupata vifaa kuvua katika bahari kuu.Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye pia ni...

Mwili wa afisa wa polisi wapatikana na majeraha kichwani Kibarani

Mwili wa afisa wa Polisi umepatikana umetupwa katika eneo la Kibarani hapa Mombasa. Akithibthisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo bunge la Jomvu Lydia Wanjiru amesikitishwa na mauaji ya afisa wa...

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imeandaa kongamano la nne la ‘Grow with Safaricom Business’ inayolenga wafanyabiashara wadogowadogo na wa kadri yani MSMEs katika eneo la Pwani.

Kongamano hilo limelenga kuwapa wajasiriamali maarifa yatakayowawezesha kuongeza uwezo wao kibiashara kupitia teknolojia.
Kongamano hilo pia limeawapa wanaMSMEs fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu jinsi gani wanaweza kutumia teknolojia ya dijiti ili kuongeza ufikiaji wao wa soko, kurahisisha shughuli, na utengenezaji uwepo thabiti mtandaoni.
Akizungumza katika kongamano hilo, afisaa mkuu wa masuala ya biashara katika kampuni yamawasiliano ya Safaricom Cynthia Kropac amesema wafanyibiashara hao wanapitia changamoto nyingi zinazozuia ukuaji wa biashara hizo.
"Pamoja na mchango mkubwa wa MSMEs katika uchumi, wanaendelea kukumbana nao changamoto kama vile ukosefu wa ujuzi na maarifa na mabadiliko ya haraka katika teknolojia miongoni mwa mengine ambayo yanazuia ukuaji wa biashara zao. Safaricom, tunaamini nguvu ya teknolojia na uwezo wake wa kubadilisha biashara, ndiyo maana tunakaribisha kampuni ya Grow with Safaricom Business ili kuwawezesha Wafanyabiashara hao,” alisema Cynthia
Kwa upande wake, mfanyibiashara wa nguo za rejareja Doreen Maore amesema kuwa kongamano hilo limemsaidia kufungua mawazo ya namna ya kukuza biashara yake.
“Kwa kongamano hili nimejifunza jinsi ambavyo nitauza bidhaa zangu nje ya Mombasa na kufikia masoko ya kimataifa. Mafunzo kuhusu masuala ya teknolojia yatanisaidia kujiendeleza na kufanya biashara yangu kuwa salama mtandaoni” alisema Doreen.
Mohammed Hersi ambae ni mtaalam wa maswala ya biashara katika sekta ya utalii amepongeza hatua ya Safaricom kuwawezesha wafanyi bishara wadogo kwa kuwapatia fursa ya kupata mafunzo yanayohusiana na biashara zao.
Aidha Hersi amesema kuwa kupitia mpango huo Safaricom imeweka wazi kuwa iko tayari kusaidia biashara zengine kukuwa.
“Nadhani kongamano hili la Grow With Safaricom limetimiza malengo yake katika eneo hili la Pwani. Safaricom inatuonyesha kuwa haitaki kukuwa pekeayake na hivyo basi kushika mkono zile biashara ndogondogo na kadri” alisema Hersi.
Vile vile Hersi ameitaka serikali ya kitaifa na zile za kaunti kuweka mazingira bora kwa ajili ya ukuaji wa biashara ndogondogo.
Kongamano la Grow with Safaricom Business Ilizinduliwa Machi mwaka huu na linalenga kutoa fursa za mtandao kwa MSMEs kuungana na wenzao, wataalam wa sekta, na washirika.

RadioRahma ads