Kongamano la kujadili uchumi wa baharini lakamilika huku hamasisho zaidi zikitolewa kupiga jeki juhudi hizo

Kongamano la kujadili mbinu za kuboresha uchumi wa baharini baina ya mataifa wanachama wa IGAD limekamilika rasmi hapa jijini Mombasa.Kongamano hilo la siku nne liliwaleta pamoja wawakilishi kutoka...

Hatimaye muungano wa mabaharia nchini SUK waandaa uchaguzi wake

Hatimae Muungano wa mabaharia nchini SUK umeandaa uchaguzi wake rasmi katika ukumbi wa Licodep eneo bunge la Likoni kama ilivyoratibiwa baada ya uamuzi wa mahakama ya leba.Katika uchaguzi huo,...

Washukiwa watatu wa uhalifu wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kombani huko Kwale baada ya kukamatwa wakitekeleza wizi wa mabavu maeneo ya kibiashara ya eneo hilo. 

Akithibitisha kukamatwa kwao naibu chifu wa Kombani Hamisi Mwamvyoga amesema kwamba watatu hao wenye umri kati ya miaka 18 na 24 wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi wa Kombani kwa miezi mitatu mfululizo sasa.

 Washukiwa hao wanaodaiwa kutumia pikipiki wakiwa wamejihami kwa silaha wamekuwa wakiwakata mapanga wenyeji kabla ya kuwaibia mali zao.

 Amewaonya vijana wanaoshirikiana na wahalifu hao kwamba watapakotambuliwa watachukuliwa hatua za kisheria kwani idara ya usalama eneo hilo inalenga kukomesha visa vya uhalifu.


RadioRahma ads