Mwili wa afisa wa polisi wapatikana na majeraha kichwani Kibarani

Mwili wa afisa wa Polisi umepatikana umetupwa katika eneo la Kibarani hapa Mombasa. Akithibthisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo bunge la Jomvu Lydia Wanjiru amesikitishwa na mauaji ya afisa wa...

Serikali ya kitaifa na kaunti zatakiwa kushirikiana kuwawezesha wavuvi kwa vifaa vya kisasa

Ipo haja ya serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushirikiana kuhakikisha inawekeza zaidi kwa kuwawezesha wavuvi kupata vifaa kuvua katika bahari kuu.Gavana wa Lamu Issa Timamy ambaye pia ni...

Rais William Ruto anaitaka mahakama kufutilia mbali jina lake katika kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa Azimio Raila Odinga kupinga kubuniwa kwa tume ya mahakama kuchunguza vifo vya waumini wa dini ya Shakahola.

Katika hati ya kiapo, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi anahoji kuwa Rais aliyeko madarakani hawezi kukabiliwa na kesi zozote za mahakama.

Akinukuu uamuzi wa Mahakama ya Juu, Muturi aliambia mahakama kuwa rais anaweza tu kushtakiwa kupitia afisi ya mwanasheria mkuu.

Akitupilia mbali kesi hiyo, AG alimweleza jaji wa Mahakama Kuu Lawrence Mugambi kwamba ombi hilo halina kipengele muhimu cha ni kwa nini tume hiyo inapaswa kusimamishwa kutekeleza majukumu yake.

Kesi hiyo itasikizwa Jumatatu wiki ijayo.


RadioRahma ads