Gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema kuwa uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji katika eneo la Melikubwa huko Macknon unalenga kukabiliana na baa la njaa katika eneo hilo ambalo hukumbwa na kiangazi kikali mara kwa mara.
Kulingana na Achani mradi huo utawasaidia wakaazi kupata maji ya mifugo na kuyatumia katika maswala ya kilimo badala ya kutegemea chakula cha msaada kutoka kwa serikali na wahisani.
Akizungumza katika eneo hilo, Achani amesema kuwa wakaazi watapata kuzalisha chakula cha kutosha kwa kuzingatia kilimo cha unyunyuziaji maji mashamba.
Kwa upande wao baadhi ya wakaazi eneo hilo wamedai kuhangaikia bidhaa hiyo muhimu kwa kutembea mwendo mrefu.
Hata hivyo wakaazi hao wakiongozwa na Mwajoto Mwagawari wamesema kwamba watatumia mradi huo hususan kufanya ukulima.