Waziri wa madini na masuala ya uchumi wa bahari Salim Mvurya ameutetea mswada wa fedha wa mwaka 2023 akisema kuwa unalenga kupunguza gharama ya maisha.
Mvurya amewataka wale wanaopinga mswada huo kuusoma kwa kina badala ya kulalamika.
Waziri huyo amesema kuwa tayari serikali imeondoa ushuru kwa bidhaa mbali mbali kama njia moja ya kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi nchini.
Aidha Mvurya amesema kuwa wananchi watapewa fursa ya kuchangia maoni ili kurekebisha mswada huo kulingana na katiba.
Haya yanajiri huku mswada huo ulioidhinishwa na baraza la mawaziri ukitarajiwa kujadiliwa na wabunge baada ya kuwasilishwa bungeni.